Exodus 4:2-5

2 aNdipo Bwana akamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?”

Akajibu, “Fimbo.”

3 b Bwana akasema, “Itupe chini.”

Musa akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia.
4Kisha Bwana akamwambia, “Nyoosha mkono wako umkamate mkiani.” Basi Musa akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 5 c Bwana akasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Bwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.”

Copyright information for SwhKC